Genesis 36:31-36

31Wafuatao ni wafalme waliotawala Edomu kabla ya mfalme yeyote wa Israeli kutawala: 32Bela mwana wa Beori alikuwa mfalme wa Edomu. Mji wake uliitwa Dinhaba.
33Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akawa mfalme baada yake.
34Yobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akawa mfalme baada yake.
35Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi.
36Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akawa mfalme baada yake.
Copyright information for SwhKC